Joshua 19:24-31

Mgawo Kwa Asheri

24 aKura ya tano ikaangukia kabila la Asheri, ukoo kwa ukoo. 25 bEneo lao lilijumuisha:

Helkathi, Hali, Beteni, Akishafu,
26 cAlameleki, Amadi na Mishali. Upande wa magharibi mpaka uligusa Karmeli na Shihor-Libnathi. 27 dTena ukageuka mashariki kuelekea Beth-Dagoni, ukagusa Zabuloni na Bonde la Ifta-Eli, ukaenda upande wa kaskazini hadi Beth-Emeki na Neyeli, ukipitia Kabul upande wa kushoto. 28 eUkaendelea hadi Abdoni, Rehobu, Hamoni na Kana, na kufika Sidoni Kuu. 29 fMpaka huo ukageukia nyuma kuelekea Rama na kwenda hadi kwenye mji wenye ngome wa Tiro, ukageuka kuelekea Hosa na kutokeza baharini katika eneo la Akzibu, 30 gUma, Afeki na Rehobu. Ilikuwepo miji ishirini na miwili, pamoja na vijiji vyake.
31 hMiji hii pamoja na vijiji vyake ilikuwa ndio urithi wa kabila la Asheri, ukoo kwa ukoo.

Copyright information for SwhNEN